Kwingineko

Harry Kane atwaa Ballon D’OR 2026

LONDON: MSHAMBULIAJI wa Bayern Munich na nahodha wa timu ya taifa ya England, Harry Kane, ametwaa tuzo ya Ballon d’Or 2026, inayotolewa kwa mchezaji bora wa soka la wanaume duniani.

Harry Kane, pia amezishukuru klabu za Tottenham Hotspur na Bayern Munich, pamoja na makocha, wachezaji wenzake na familia yake, kwa mchango wao katika safari yake ya soka na mafanikio aliyoyapata hadi kubeba tuzo hiyo kubwa duniani.

Kane alisema mafanikio yake hayajapatikana kwa juhudi zake pekee, bali pia kutokana na msaada wa watu na taasisi mbalimbali zilizomsaidia kukua na kuimarika katika soka.

Alitambua mchango wa Tottenham Hotspur, klabu aliyochezea kwa miaka kadhaa kabla ya kujiunga na Bayern Munich mwaka 2023, akieleza umuhimu wa hatua hiyo katika kujenga msingi wa mafanikio yake.

Aidha, aliishukuru Bayern Munich kwa kumpa nafasi ya kuendelea kuonyesha uwezo wake na kushindana katika kiwango cha juu cha soka la Ulaya.

Kane pia alitoa shukrani kwa makocha na wachezaji wenzake kwa ushirikiano wao, akisisitiza kuwa mafanikio katika soka yanahitaji mshikamano na juhudi za pamoja.

Alimshukuru pia familia yake kwa kuwa sehemu muhimu ya safari yake, hasa katika kipindi ambacho amekuwa akikabiliana na changamoto na matarajio makubwa ya mashabiki.

Kauli hiyo inaonyesha namna Kane anavyothamini mchango wa klabu na watu mbalimbali katika safari yake ya soka, huku akiendelea kujijengea jina kama mmoja wa washambuliaji wanaotambulika katika soka la Ulaya.

Tuzo hiyo iliyonyakuliwa na HerryKane ni tuzo ya 70 tangu kutolewa kwa tuzo hiyo. MSHAMBULIAJI wa Bayern Munich, Harry Kane, ametoa ujumbe maalumu wa kumtakia heri kocha wake, Vincent Kompany, ambaye hakuweza kuhudhuria hafla hiyo kutokana na hali yake ya kiafya.

Kane alisema alitumaini tuzo hiyo ingekuwa chanzo cha faraja na kumpa nguvu Kompany katika kipindi hicho, akitambua mchango wa kocha huyo katika mafanikio yake na ya timu.

Ujumbe huo ulidhihirisha uhusiano mzuri uliopo kati ya Kane na Kompany, huku mshambuliaji huyo akitumia fursa hiyo kuonyesha kuthamini mchango wa kocha wake katika safari yao ya soka.

Related Articles

Back to top button