Nyumbani

Singida kuweka kambi Dar kuimaliza Tusker

DAR ES SALAAM: KOCHA wa Singida Black Stars, Kimoto Papy, amesema kikosi chake kitaweka kambi Dar es Salaam kujiandaa na mchezo wa marudiano dhidi ya Tusker ya Kenya utakaochezwa Oktoba 25, mwaka huu.

Singida inaingia katika mchezo huo ikiwa na faida ya ushindi wa bao 1-0 iliyoupata ugenini katika mchezo wa kwanza, lakini Kimoto amesema bado wana kazi ya kufanya kuhakikisha wanamaliza jukumu hilo kwa mafanikio.

Kocha huyo amesema maandalizi ya mchezo huo ni muhimu, akisisitiza kuwa wachezaji wanahitaji kupumzika vizuri na kufanya kazi kwa bidii ili kufikia kiwango kinachohitajika katika mchezo wa marudiano.

Kimoto pia amekiri kuwa changamoto aliyokutana nayo ni kutowafahamu vizuri wachezaji wake kutokana na muda mfupi wa maandalizi ya msimu huu, hivyo bado anahitaji muda wa kuwajenga na kuwaingiza katika falsafa yake ya soka.

Amesema licha ya changamoto hiyo, ameanza kuona uwezo wa wachezaji alionao, huku akifurahishwa na ari na moyo wa kupambana walioonesha, katika mchezo uliopita.

Related Articles

Back to top button