Afrika Mashariki

Hello Mr. Right Kenya yamtambulisha mtangazaji mpya

NAIROBI: BAADA ya wiki kadhaa za minong’ono na mijadala kwenye mitandao ya kijamii, hatimaye fumbo limefumbuliwa. Mwigizaji, mwanamitindo na mtayarishaji wa maudhui Trisha Khalid ametambulishwa kuwa mtangazaji mpya mwenza wa kipindi maarufu cha Hello Mr. Right Kenya, kinachoingia msimu wake wa tano.

Trisha ataungana na mtangazaji Dr. Ofweneke pamoja na mtaalamu wa mahusiano Getrude Mungai, katika msimu mpya wa kipindi hicho kinachowakutanisha watu wanaotafuta wapenzi na wenza wa maisha.

Trisha alitambulishwa rasmi jana katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Victoria Towers, Upper Hill, Nairobi, ambapo alipokelewa kwa shangwe.

Anachukua nafasi iliyoachwa na Risper Faith, aliyekuwa mtangazaji mwenza katika msimu wa nne.
Watayarishaji wa kipindi hicho wamesema uteuzi wa Trisha unaendana na mabadiliko ya tasnia ya burudani nchini Kenya, huku akiwakilisha kizazi kipya cha mastaa wenye ushawishi mkubwa mitandaoni.

Mbali na kazi yake ya uigizaji na uanamitindo, Trisha amejijengea jina kupitia mitandao ya kijamii na uwezo wake wa kuvutia mijadala na kufuatiliwa na mashabiki wengi.

Dr. Ofweneke alisema timu ya uzalishaji ilikuwa na majina kadhaa kabla ya kumchagua Trisha.
“Tulikuwa na majina takribani matano. Tuliangalia utu, nguvu, uhalisia, ubunifu, pamoja na mtazamo wa kila mmoja kuhusu mapenzi na ndoa. Mwisho wa yote, kila kitu kilimuelekea Trisha Khalid,” alisema.

Akaongeza kwa utani:
“Binafsi, najua nitafurahia sana msimu huu.”
“Niko tayari kumstress Dr. Ofweneke”
Kwa upande wake, Trisha amesema yuko tayari kuleta nguvu na burudani zaidi katika kipindi hicho, huku akimtania Dr. Ofweneke kwamba msimu huu hatakuwa na amani.

“Nitawekeza nguvu zaidi na burudani zaidi kutoka kwetu sote. Niko tayari kumstress Dr. Ofweneke,” alisema Trisha.

StarTimes yaeleza sababu ya kumchagua
StarTimes imesema uteuzi wa Trisha ulifanywa kwa kuzingatia umaarufu wake, uzoefu na uwezo wa kuwasiliana na watazamaji.

Related Articles

Back to top button