Nyumbani

Evans Mgeusa Katibu Mkuu mpya TFF

DAR ES SALAAM: SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limefanya uteuzi wa Katibu Mkuu mpya, Evans Mgeusa pamoja na kufanya mabadiliko katika baadhi ya kurugenzi zake.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na shirikisho hilo, imefafanua teuzi hizo zimetangazwa leo Jumatatu katika kikao cha Kamati ya Utendaji chini ya Rais wa TFF, Wallace Karia.

Kwa muktadha huo, Mgeusa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Njombe (NJOREFA), sasa anachukua nafasi ya Oscar Mirambo aliyekuwa akikaimu wadhifa huo.

Na Mirambo ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu wakati Mustapha Yusuph anakuwa Mkurugenzi wa Fedha.

Mabadiliko mengine yanahusisha sekta ya Kurugenzi ya Sheria, Habari na Masoko ambapo imegawanywa na kuwa kurugenzi tatu tofauti.

Walioteuliwa kuongoza kurugenzi hizo ni Hassan Njama (Biashara na Masoko), Boniface Wambura (Sheria), na Cliford Ndimbo (Habari na Mawasiliano).

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button