Ligi Ya WanawakeNyumbani
Simba vs Fountain mechi ya kibabe wanawake

LIGI Kuu ya Soka ya Wanawake Tanzania Bara inaendeleoa kwa michezo mitatu katika mikoa ya Dar es Salaam, Dodoma na Iringa.
Simba Queens itakuwa wenyeji wa Fountain Gate Princess kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Katika mechi nyingine The Tigers Queens itakuwa mgeni wa Baobab Queens kwenye uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Nayo Mkwakwa Queens itakuwa mwenyeji wa Amani Queens kwenye uwanja wa Samora mjini Iringa.