Mastaa

Baby Ollie awashangaza mashabiki kwa ukuaji wa haraka

DAR ES SALAAM: MISS Tanzania wa zamani na msanii wa filamu nchini, Wema Sepetu, amewashangaza mashabiki wake baada ya kufichua kuwa mwanawe, Baby Ollie, mwenye umri wa miezi miwili, tayari anavaa nguo zinazolingana na watoto wenye umri wa kati ya miezi tisa na 12.

Wema alionesha picha za mwanae kupitia mitandao ya kijamii, akieleza kufurahishwa kwake na afya pamoja na ukuaji wa mtoto huyo.

Katika ujumbe wake, msanii huyo alisema Baby Ollie anaendelea kukua kwa kasi, jambo alilolihusisha na hali yake nzuri kiafya.

“My healthy baby boy… Tunavaa nguo za 9-12 months… Na wakati ndo kwanza tuna 2 months… Nyie kweza,” aliandika Wema katika ujumbe huo, akionesha mshangao wake kutokana na ukubwa wa mwanawe licha ya kuwa na umri mdogo.

Kauli hiyo ilizua gumzo miongoni mwa wafuasi wake, ambapo baadhi walionesha mshangao wao na wengine wakisema ukuaji huo ni jambo la kufurahisha. Wema pia ameendelea kushirikisha mashabiki wake hatua mbalimbali za ukuaji wa mwanawe, ambaye tangu kuzaliwa kwake amekuwa akivuta hisia za wengi ndani na nje ya Tanzania.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button