Kikapu

Dar City yaendeleza ubabe ligi ya mkoa

DAR ES SALAAM: Timu ya mpira wa kikapu ya Dar City imeendelea kuonesha ubabe katika Ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam baada ya kuifunga Pazi vikapu 66-51 katika mchezo uliopigwa jana.

Mchezo huo ulikuwa wa ushindani mkubwa, huku kila timu ikipambana kusaka ushindi tangu mwanzo hadi mwisho.

Hata hivyo, Dar City ilitumia ubora wake kuondoka na ushindi muhimu uliowafanya kuendelea kuongoza msimamo wa ligi.

Kwa ushindi huo, Dar City sasa imecheza jumla ya mechi tisa na kushinda zote, ikiendelea kubaki kileleni mwa msimamo wa Ligi ya Mkoa wa Dar es Salaam bila kupoteza hata mchezo mmoja.

Kwa upande wa Pazi, kipigo hicho kimekatiza rekodi yao nzuri na kuwafanya kubaki katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi baada ya kupoteza mchezo huo muhimu.

Related Articles

Back to top button