Ligi KuuNyumbani

Mpole ni mchezaji huru

KLABU ya soka ya Geita Gold imefikia makubaliano ya kusitisha mkataba na aliekuwa mchezaji wake George Mpole kuanzia leo.

Barua ya Geita Gold iliyotolewa na Mtendaji Msaidizi wa klabu Ramadhan Bukambu ameelezea hatua hiyo.

“Uongozi wa Klabu ya Geita Gold unakutaarifu rasmi ya kwamba mkataba wako wa ajira kati ya klabu na wewe umemalzika rasmi leo baada ya pande mbili kukubaliana na uko huru kujiunga na klabu yoyote kuanzia leo”,imesema sehemu ya barua hiyo.

Geita imesema uongozi umefikia hatua hiyo baada ya kuzungumza na mchezaji kwa kina na kufikia makubaliano hayo kwa maslahi mapana ya klabu na mchezaji mwenyewe.

Akizungumza na Spotileo Mpole amesema:“Ni kweli mimi na timu yangu ya Geita tumefikia makubaliano ya kusitisha mkataba na hiyo ni kutokana na kutaka kwenda kujitibia zaidi baada ya kutokuwa sawa kiafya tangu msimu huu umeanza.”

Mpole aliibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2020/21 akifunga mabao 17 mbele ya Fiston Mayele wa Yanga aliyefunga mabao 16.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button