Nyumbani

Simba yatinga Ikulu Zanzibar

ZANZIBAR: VIONGOZI na benchi la ufundi na wachezaji wamepata nafasi ya kukutana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi leo mchana baada ya kuwasili visiwani Zanzibar.

Katika hafla hiyo fupi iliyofanyika Ikulu Simba wamemkabidhi zawadi ya jezi Dkt. Mwinyi pamoja na mke wake mama Mariam Mwinyi.

Akizungumzia katika hafla hiyo fupi Dkt. Mwinyi amewapongeza kwa namna walivyowakilisha vyema nchi kimataifa jambo linasaidia kukuza utalii kupitia michezo.

Amesema serikali yake imejipanga kuendelea kuboresha na kujenga viwanja vya michezo vitakuwa na vigezo vya kutumika michuano ya AFCON 2027 na CHAN 2025.

“Kutukaribisha muda wowote kuja kuchezea hapa michezo ya mashindano ya ndani na kimataifa,” amesema Dkt. Mwinyi.

Mwenyekiti wa Simba, Murtaza Mangungu amempongeza Dkt. Mwinyi kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuleta maendele.

Mangungu ametumia nafasi hiyo kuwasilisha ombi la Simba kupata eneo ambalo tutajenga kituo cha kukuzia vipaji vya mpira wa miguu (academy).

 

 

 

 

 

 

Related Articles

Back to top button