Ligi KuuNyumbani

Coastal kuizuia Simba leo?

LIGI Kuu ya soka Tanzania Bara inaendelea leo kwa michezo miwili kupigwa Tanga na Singida.

‘Wekundu wa Msimbazi’, Simba ni wageni wa ‘Wagosi wa Kaya’, Coastal Union kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Simba inashika nafasi ya 3 katika msimamo wa ligi ikiwa pointi 31 baada ya michezo 14 wakati Coastal ipo nafasi ya 12 ikiwa na pointi 12 baada ya michezo 13.

Baada ya kuifunga Coastal kwenye uwanja wa Mkwakwani bao 1-0, ‘Walima Zabuni’, Dodoma Jiji itakuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Liti mjini Singida.

Dodoma Jiji ipo nafasi ya 13 ikiwa na pointi 12 baada ya michezo 14 wakati Ruvu Shooting ni ya 15 ikiwa na pointi 11 baada ya michezo 14.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button