Ayamaami yaibamiza Mnara 2-1 NMB Cup
TIMU ya Ayamaami imeanza vyema mashindano ya soka kuwania kombe la NMB yanayoendelea katika uwanja wa Halmashauri Mbulu Mjini mkoani Manyara.
Katika mchezo wa ufunguzi Ayamaami imefanikiwa kuichakaza Mnara kwa magoli 2-1.
Akifungua michuano hiyo Meneja wa Benki ya NMB wilayani Mbulu mahmud Mtengela amesema wataendelea kuunga mkono michezo kwani imekuwa ikitoa ajira kwa vijana na inadumisha upendo na kujenga umoja.
“Huu ni mwanzo tu na tutafanya mengi katika wilaya yetu lengo kuibua vipaji,”amesema Mtengela.
Jumla ya timu nane zinashiriki mashindano hayo kuwania NMB Mbulu Cup ambayo yameanza Mei 18 hadi Mei 27 mwaka huu.
Michuano hiyo imeandaliwa na Chama cha Soka Wilaya ya Mbulu kushirikiana na Halamashauri ya mji wa Mbulu na kudhaminiwa na benki ya NMB.
Naye Ofisa michezo halmashauri ya mji wa Mbulu Benson Maneno amesema mbali na kuibua vipaji mashindano hayo yatasaidia pia kuhamasisha timu zilizopo wilayani humo kujitokeza na kujisajili ili zitambulike na msajili kwani zipo nyingi ila hazijasajiliwa.
Amefafanua kuwa michuano hiyo itaendeshwa kwa mfumo wa makundi na baadae robo fainali, nusu fainali na fainali.
Timu zinazoshiriki ni Mnara FC,Ayamaami FC, Sanu,Endagikoti,Bargish FC,Tango FC , Home boys, Daudi FC
Zawadi kwa washindi zitatolewa ambapo mshindi wa kwanza atazawadiwa Sh 500,000 pamoja na kombe,mshindi wa pili laki 300,000 pamoja na kombe na mshindi wa tatu atapata laki 200,000 na kombe, pia kutakuwa na zawadi kwa mfungaji mwamuzi bora.