Ligi KuuNyumbani

Gadiel afungiwa kwa kumwaga ‘unga’ uwanjani

MCHEZAJI wa timu ya Simba Gadiel Michael amefungiwa michezo mitatu na kutozwa faini ya sh 500,000 kwa kosa la kulazimisha kuingia na kumwaga vitu vyenye asili ya unga katikati ya uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.

Taarifa ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania(TPLB) imesema Gadiel alilazimisha kuingia uwanjani saa 4.25 asubuhi siku ya mchezo kati ya Mbeya City na Simba Novemba 23, 2022 kwa kile alichoeleza alitaka kukagua uwanja.

TPLB imesema licha ya walinzi wa uwanja huo kumzuia Gadiel (ambaye alikuwa ameongozana na watu kadhaa waliovalia fulana zenye nembo ya klabu ya Simba) kwa sababu haukuwa muda rasmi wa zoezi hilo na Simba haikufanya mawasiliano yoyote na kamishna wala mratibu wa mchezo wakieleza jambo hilo, Gadiel alitumia hila na kufanikiwa kuwakwepa walinzi kisha kuingia uwanjani.

Kwa mujibu wa bodi hiyo ya ligi mchezaji huyo alipoingia uwajani hakuonesha dalili yoyote ya kukagua eneo la kuchezea badala yake alionekana kwenda moja kwa moja hadi eneo la katikati ya kiwanja na kumwaga unga huo.

TPLB imesema adhabu hiyo ni kwa kuzingatia kanuni ya 41:5(5.5) ya ligi kuu kuhusu udhibiti kwa wachezaji.

Related Articles

Back to top button