Mastaa

Davido atoa pole kwa WanaKebbi

LAGOS: NYOTA wa muziki wa Nigeria David Adeleke maarufu Davido, ametuma ujumbe wa faraja kwa familia za wasichana waliotekwa katika Jimbo la Kebbi nchini Nigeria.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Davido ameeleza masikitiko yake ya kutekwa kwa wasichana hao wa Kebbi huku akiwaomba Wanigeria wote waungane na kuwa na umoja kuhakikisha watoto ambao hawajatekwa wawe na amani na wawaondolee hofu.

“Moyo wangu uwafikie watoto wadogo wa kike waliotekwa Kebbi pamoja na familia zao. Hakuna familia inayopaswa kupitia haya. Kama Nigeria tunatakiwa kusimama Pamoja na kuungana na kuendelea ili kila mtoto akue katika mazingira ya amani na matumaini” amesema Davido

Davido amewaomba Wanigeria wafanye kila liwezekanalo ili kuwarudisha wasichana wa Kebbi salama nyumbani.

“Ninawaomba yeyote mwenye taarifa za kuaminika ajitokeze kwa njia yoyote salama na yenye uwajibikaji wawezavyo,ili kuunga mkono juhudi zinazoendelea za kuwaokoa” amesema Davido

Ingawa maelezo kamili kuhusu ujumbe wa Davido si mengi, kitendo chake kinaonesha kwamba wasanii wanaweza kutumia majukwaa yao kuwafariji wengine katika nyakati ngumu.

Related Articles

Back to top button