
LIGI Kuu ya Soka Tanzania Bara inaendelea leo kwa mchezo mmoja mkoani Tanga.
Wakosi wa Kaya, Coastal Union ni wenyeji wa Dodoma Jiji kwenye uwanja wa Mkwakwani.
Coastal Union inashika nafasi ya 12 katika msimamo wa ligi ikiwa na pointi 12 baada ya michezo 14 wakati Dodoma Jiji ipo nafasi ya 16 mwisho wa msimamo ikiwa na pointi 9 baada ya michezo 13.
Akizungumza Novemba 29 kuelekea mchezo huo Kocha Msaidizi wa Dodoma Jiji Kassim Liyogope amesema kikosi chake kipo tayari kusaka pointi 3 muhimu.
“Tumechukua tahadhali zote kuhakikisha tunapata matokeo katika mchezo wa kesho,” amesema Liyogope.
Novemba 29 kumefanyika mchezo mmoja mkoani Mbeya ambapo vinara wa ligi kuu, Yanga imepoteza mchezo wa kwanza baada ya kutofungwa katika mechi 49 ilipokutana na kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Ihefu.