Kwingineko

Kocha ajitetea kumuweka Salah benchi

"Bado ni mchezaji muhimu kwetu"

FRANKFURT:KOCHA wa Liverpool Arne Slot, amezungumzia uamuzi wake wa kumwacha nje nyota Mohamed Salah kwenye mechi mbili mfululizo za Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza tangu 2017.
Slot amesema haikuwa rahisi kumwacha Salah benchi, lakini amesisitiza hilo ni kutokana na ushindani mkubwa ndani ya kikosi chake.
“Ndiyo, ilikuwa ngumu. Lakini nina wachezaji wengi wazuri sana, na kila mara ninapochagua kikosi ni changamoto,” alisema.
Ameeleza kuwa uamuzi huo pia ulihusishwa na jinsi walivyomaliza mchezo dhidi ya Manchester United, pamoja na mabadiliko aliyofanya kufuatia majeraha ya Ryan.
“Nilipenda jinsi tulivyomaliza mechi ile, tulitengeneza nafasi nyingi. Na kutokana na Ryan kuwa nje, tulilazimika kubadilisha muundo wa kiungo wetu. Mo bado ni mchezaji muhimu, hata kama anaianza mechi kutoka benchi,” amesema Slot.

Related Articles

Back to top button