Kwingineko

Nagelsmann kuwa kocha mpya Ujerumani

JULIAN Nagelsmann anatarajiwa kutangazwa Kocha mpya wa timu ya taifa ya soka ya wanaume ya Ujerumani.

Anatarajiwa kuteuliwa kwa mkataba wa muda mfupi hadi michuano ya Euro 2024, ambayo Ujerumani itakuwa mwenyeji.

Nagelsmann mwenye umri wa miaka 36 atachukua nafasi ya Hansi Flick, aliyetimuliwa Septemba 10 kufuatia Ujerumani kupokea kichapo cha mabao 4-1 kutoka kwa Japan katika mechi ya kirafiki ya kimataifa.

Hakuwa kwenye nafasi yoyote ya ukocha tangu alipooneshwa mlango wa kutokea Bayern Munich Machi mwaka huu.

Michuano ya Euro 2014 itaanza Juni 14, 2024 ambapo Nagelsmann atakuwa na mechi tatu za kirafiki za kimataifa kati ya sasa na michuano hiyo.

 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button