EPL

Nuno Espírito Santo atimuliwa na Nottingham Forest

ENGLAND:NOTTINGHAM Forest wamemtimua kocha wao Nuno Espírito Santo baada ya mechi tatu tu za Premier League msimu huu. Inaelezwa kuwa uhusiano wake na mmiliki wa timu, Evangelos Marinakis ulichafuka, jambo lililomgharimu kibarua chake, licha ya mafanikio makubwa msimu uliopita alipoipeleka timu hadi nafasi ya 7 na kuirudisha Ulaya mara ya kwanza baada ya miaka 30.

Kwa muda aliokaa City Ground, Santo aliiongoza Forest kwenye michezo 73, akishinda 28, sare 20 na kufungwa mara 25. Mashabiki wengi wanahisi ametimuliwa vibaya, hasa ukizingatia maendeleo aliyowapa.

Sasa Forest wanatafuta kocha mpya, majina yanayotajwa ni Oliver Glasner, Andoni Iraola, Mauricio Pochettino, Marco Silva na Ange Postecoglou.

Related Articles

Back to top button