Unyanyasaji ulivyoharibu ndoa ya Karisma Kapoor, Sunjay Kapur

DELHI:NAMNA ndoa ya muigizaji wa filamu nchini India Karisma Kapoor na mfanyabiashara Sunjay Kapur ilivyovunjika, imeewekwa wazi kwamba sababu ilikuwa ni mgogoro mkubwa wa madai ya unyanyasaji na kifedha.
Karisma Kapoor, mmoja wa waigizaji mashuhuri zaidi wa miaka ya 1990, alijulikana katika filamu ‘Raja Hindustani’, ‘Dil To Pagal Hai’, ‘Biwi No. 1’, na ‘Zubeidaa’.
Karisma amesema mwaka 2003, alifunga ndoa na mfanyabiashara Sunjay Kapur kwenye makazi yake huko Delhi, lakini muungano wao ulisambaratika haraka, na hatimaye kupelekea vita vya hadharani na vikali vya talaka kuanzia mwaka 2014.
Ingawa wanandoa hao hapo awali waliwasilisha talaka kwa makubaliano ya pande zote mbili, kesi hiyo iliongezeka na kuwa vita mbaya ya kisheria iliyojaa madai mazito.
Katika ombi lake la talaka, Karisma alimshutumu Sunjay kwa unyanyasaji wa kimwili na kiakili. Moja ya madai yaliyosumbua zaidi ni kwamba wakati wa fungate yao, Sunjay alidaiwa kumlazimisha kulala na marafiki zake. Karisma pia alidai kuwa wakati wa ujauzito wake, Sunjay alidaiwa kumtaka mama yake ampige kofi kwa sababu hangeweza kuingia kwenye nguo ambayo mama mkwe wake alitaka avae.
Babake Karisma ambaye ni muigizaji mkongwe Randhir Kapoor, akizungumza na Hindustan Times, alitoa ujumbe kwamba “Sunjay ni mtu wa daraja la tatu … Hatuhitaji kukimbilia pesa za mtu yeyote. Kipaji chetu kinatosha kutusaidia maishani.”
Pia Karisma alidai kuwa Sunjay hakuwa tayari kutoa msaada wa kifedha kwa watoto wao. Hii ilimpelekea kuwasilisha malalamiko ya unyanyasaji wa nyumbani dhidi ya Sunjay na mama yake. Baadaye polisi walianzisha uchunguzi kuhusu suala hilo.
Hatimaye, wanandoa hao walifikia makubaliano ya kisheria na wakapewa talaka mwaka 2016. Ripoti zilionyesha kuwa Karisma alipokea nyumba huko Khar na Sunjay alikubali kuwekeza Rs 14 crore katika bondi kwa watoto wao, na kutoa takriban laki 10 kwa riba ya kila mwezi.
Hata hivyo Sunjay Kapur aliaga dunia Juni 12, 2025, katika jiji la London nchini Uingereza kutokana na mshtuko wa moyo, unaoripotiwa kuwa ulisababishwa na mzio baada ya kumeza nyuki kimakosa wakati wa mechi ya polo.