Singida Black Stars watamba kumfunga Yanga, kubeba FA

BABATI:MCHEZAJI bora wa mechi ya fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB kati ya Simba na Singida Black Stars, Emanuel Kwame amesema ushindi wa 3-1 dhidi ya Simba umewapa nguvu ya kuamini kwamba wataifunga Yanga na kubeba Kombe la Shirikisho.
Matumaini hayo yamekuja baada ya Singida Black Satrs kushinda bao 3-1 dhidi ya Simba SC katika mechi iliyopigwa leo Uwanja wa Tanzanite huko Babati.
Kwame amesema hawatopoteza mchezo huo watacheza kwa juhudi kubwa na kwa kucheza kwa timu kama walivyocheza dhidi ya Simba na wanatumaini kusishinda Yanga.
“Hatuwezi kupoteza tulijipanga kucheza hivi na kushinda na tunashukuru tumeshinda, tunaimani tutaishinda Yanga na tutabeba kombe la Shirikisho katika fainali.” Amesema.
Awali Kocha wa Singida Black Stars David Ouma amesema namna timu hiyo ilivyocheza na Simba ndiyo kiwango chao wanachotakiwa kucheza katika mechi zote hivyo watacheza kwa kiwango hicho katika mechi ya Yanga na wanaimani watabeba kombe hilo kwa kuifunga Yanga.
“Hiki ndicho kiwango ambacho tunatakiwa kucheza na nawataka wachezaji wangu wajitunze na hiki ndicho kiwango chetu. Tunatakiwa kucheza mechi zote namna hii, na mechi ya fainali tunaamini tunabeba kombe.” Ameeleza.