Burudani

Wasanii watakiwa kutumia filamu na tamthilia kuelimisha jamii

DAR ES SALAAM:WANII nchini wametakiwa kutumia Filamu na Tamthilia kama njia ya kuelimisha na kuhasa jamii, badala ya kuzitumia vibaya na kupotosha maadili ya kitanzania.

Wito huo umetolewa na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Gervas Kasiga ‘Chuma’, ambapo amesisitiza kuwa Filamu zikilindwa na kuendelezwa ipasavyo, zinaweza kuibua fursa kwa wasanii, kukuza ajira, na kuongeza pato la Taifa.

“Filamu ni nyenzo muhimu sana katika kujenga taswira ya Mtanzania. Tangu enzi za ukoloni, filamu zimekuwa zikichangia katika kuibua mijadala muhimu kuhusu jamii yetu,” alisema Kasiga.

Ameongeza kuwa endapo filamu zitakosa mwelekeo mzuri, zinaweza kusababisha madhara makubwa kwa jamii, lakini zikitumika kwa njia sahihi, zitachochea mabadiliko chanya.

Amesema pia kuwa ulasimishaji wa biashara ya filamu pamoja na kuwahusisha wazalishaji wa ndani na nje ya nchi, kutachochea maendeleo ya sekta hiyo huku miswada ya kazi ikilindwa na kutozwa kwa mujibu wa sheria.

Kasiga ameongeza kuwa sekta ya filamu ina nafasi kubwa katika kutangaza Utamaduni na Lugha ya Kiswahili, si tu ndani ya nchi bali hata katika ngazi ya kimataifa.

Related Articles

Back to top button