Nyumbani

Pacome, Max, Aziz Ki kukiwasha Singida

DAR ES SALAAM: KIKOSI cha Yanga  kinatarajiwa kushuka dimbani kikiwa kamili dhidi ya Singida Black Stars katika mchezo maalum wa uzinduzi wa uwanja mpya wa Singida Black Stars huko Singida.

Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe, amesema kuwa timu yao itaingia uwanjani ikiwa na mastaa wake wote waliopo, akiwemo Stephen Aziz Ki, Pacome Zouzoua, na Max Nzengeli, huku wale waliopo kwenye majukumu ya timu za taifa wakikosekana.

“Tunaondoka Dar es Salaam siku ya Jumamosi, Machi 22, kwa usafiri wa SGR hadi Dodoma, kisha tutaendelea na gari maalum kuelekea Singida, tunakwenda tukiwa kamili, tukiwa na nyota wetu kama Aziz Ki, Pacome na Max,” amesema Kamwe.

Kamwe pia hakusita kueleza kwamba Yanga haitacheza kwa mzaha, akidai kuwa waliwaeleza Singida Black Stars kutafuta timu za kiwango chao, lakini waliamua kukubali changamoto.

“Sasa tunaenda kuwashona na kuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kushinda katika uwanja huo mpya,” ameongeza.

Kwa upande wa maandalizi, Kamwe amesema kuwa wachezaji ambao hawapo kwenye majukumu ya timu za taifa wanaendelea na mazoezi, wakijiandaa na michezo mbalimbali iliyo mbele yao.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button