Nyumbani
Simba yakusanya milioni 30 saa 24

DAR ES SALAAM: Wekundu wa Msimbazi Simba wamefanikiwa kukusanya Sh milioni 32 na elfu 85 katika kampeni yao ya “Tunawajibika pamoja” walioizindua rasmi jana Januari 15, 2025.
Simba ilianzisha kampeni hiyo kulipa faini inayotokana na adhabu waliyopewa na shirikisho la soka barani Afrika CAF kufuatia vurugu zilizotokea katika mchezo wa kombe la Shirikisho Afrika kati ya Simba na CS Sfaxien ya Tunisia.
Simba kama CS Sfaxien wamepigwa faini ya zaidi ya shilingi milioni 100 na kucheza mchezo mmoja bila mashabiki na hapo jana walitangaza utaratibu wa mashabiki wao kuchangia pesa hizo na muitikio unaonekana wa kuridhisha




