Nyumbani
‘Full house’ ya Yanga yamkosha Rais Samia
DAR ES SALAAM : RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan ametoa salamu za pongezi Yanga kwa kufanikisha tamasha lao na kujaza uwanja.
Amesema anajua wamejitaarisha vizuri kwa msimu ujao nimefatilia vifaa vizuri walivyosajiliwa na kuwatakia kila la kheri.
“Niko katika kikao na wazee wa Ifakara na huku nafatilia tamasha hilo katika Luninga,” amesema Rais Samia alipopiga simu kwa makamu wake.
Naye makamu wa Rais, Philip Mpango amewapongeza viongozi , benchi na wachezaji wa Yanga kwa kufanikiwa kufanya vizuri katika msimu ujao wa Mashindano.
“Kwa vifaa hivi bilivyoshushwa hapa wataweza kweli? Ninaimani msimu ujao Yanga ni bingwa na kombe la kwetu aliendi kokote,” amesema Mpango.