Filamu

Wolper awasanua wanawake

MSANII wa Filamu na Mfanyabiashara nchini Jackquline Wolper amewakumbusha wanawake kuwasaidia wanaume zao kwenye baadhi ya majukumu ya nyumbani.

Kupitia mtandao wake wa Instagram Wolper ameandika kuwa hata kama mwanaume wako anapesa kiasi gani? unapaswa kuonesha upendo kumsaidia baadhi ya majukumu.

“Wanawake hata kama mmeo anapesa kiasi gani? Onesha upendo (Show love) usimuachie kila kitu wanachokaga vile vi hela avyokupa save jamani khaa!. Umeme, Gas kama hayupo (buy) nunua”

“Kuna kaka ananileteaga vifaa vya ujenzi home juzi tu katoka kulalamika kasema mkwewe anapata mshahara mzuri sana na yeye ndio kamtafutia kazi ila amsaidii wala ajawahi mnunulia kiatu wala leso.” ameandika Wolper

Ikumbukwe Wolper ni mama wa watoto wawili na mume wake Richard maarufu kama ‘Rich Mitindo’.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button