Habari Mpya

23 waitwa Taifa Stars kuikabili Libya kirafiki

WACHEZAJI 23 wameitwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya soka(Taifa Stars) kitakachoingia kambini kwa ajili ya michezo mwili ya kirafiki dhidi ya Libya kwenye kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu(FIFA).

Kocha Mkuu wa Stars Honour Janza amewataja wachezaji hao kuwa ni Aishi Manula, Beno Kakolanya, Saidi Kipao, Kibwana Shomari, Datius Peter na David Luhende.

Wengine ni Abdulmalick Adam, Abdi Banda, Carlos Protas, Oscar Masai, Dickson Job, Abdallah Mfuko, Himid Mao, Sospeter Bajama, Mzamiru Yassin na Feisal Salum.

Wachezaji wengine walioitwa ni David Uromi, Mohamed Banka, Mbwana Samatta, Simon Msuva, Ibrahim Joshua, Salid Khamis na Habib Kyombo.

Related Articles

Back to top button