Mastaa

Zari awaombea waislamu

DAR ES SALAAM: MSANII na Mfanyabiashara, Zari Hassan ‘Zari The Boss Lady’, amefanya dua maalumu waumini wa dini ya kiislamu katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, Zari amechapisha picha mpya akiambatanisha na ujumbe wa kuwatakia mema waumini wote wanaotekeleza ibada ya funga.

Katika ujumbe huo, Zari ameandika: “Mwenyezi Mungu atujaalie rehema, nguvu na uongofu katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani, atukubalie swaumu na maombi yetu”.

 

Related Articles

Back to top button