Kwingineko

Yanga yazindua tawi Rwanda

KIGALI: KLABU ya Yanga imezindua tawi jipya Kigali nchin Rwanda na kusema wanatambua mchango mkubwa wa wanayanga wa nchini humo.

Akizungumza jijini hapa Leo kwenye uzinduzi wa tawi hilo Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji amewahimiza wanayanga kuendelea kuadhimisha mahusiano mazuri.

“Niwasihi tuendelee kudumisha mahusiano haya ambayo tumeyaanza leo nina hakika tutafika mbali zaidi , sisi viongozi wa Yanga tunathamini na kutambua mchango wa Wanayanga wa hapa Rwanda kwakuwa hata timu yetu imewahi kupata wachezaji wazuri waliyoisaidia yanga ambao wametoka katika ardhi hii kama Haruna Niyonzima, Sibomana Patrick na wengine” Arafat Hajj.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tawi la Yanga Kigali Jean Musabyimana amesema: “Tunaushukuru sana uongozi wa klabu yetu kwa kuja hapa Rwanda na kujumuika nasi, tupo tayari kuiwakilisha vyema klabu yetu hapa na tunawaahidi tutakuwa mfano wa kuigwa,” amesema.

Ibrahim Samwel wa idara ya wanachama Yanga amesema wao kama idara ya Wanachama na Mashabiki ni faraja kubwa na heshima kuona familia ya wanachama rasmi inazidi kukua na kuongezeka nje ya mipaka ya nchi.

“Tunawakaribisha sana katika familia ya mabingwa tawi hili la Yanga – Kigali ili tuijenge yanga iliyokuwa imara na yenye msuki mkubwa kiuchumi katika kufikia malengo chanya na endelevu,”amesema.

Related Articles

Back to top button