Africa
Yanga yapokea mil 10/ magoli dhidi ya Rivers

KLABU ya Yanga imepokea zawadi ya shilingi Milioni 10 kutoka kwa Rais Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa magoli mawili iliyofunga ugenini iliposhinda 2-0 katika mchezo wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la CAF dhidi ya Rivers United.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amekabidhi fedha hizo Dar es Salaam leo kwa Afisa habari wa Yanga, Ally Kamwe.
“Tunakuahidi Mama, Kazi bado haijakwisha. Jumapili ya Tarehe 30/4/ 2023 tunakwenda kupambana zaidi na kulipa heshima Taifa letu la Tanzania kwa kufuzu hatua ya Nusu Fainali,” amesema Kamwe.
Magoli yote mawili ya Yanga yalifungwa na Fiston Mayele.