Nyumbani

Yanga yalazimisha suluhu Malawi

KLABU ya Yanga leo imelazimisha suluhu dhidi ya Nyasa Big Bullets ya Malawi katika mchezo maalumu wa kirafiki wa kimataifa kuadhamisha miaka 59 ya Malawi.

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na mwenyeji wake Rais Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera wa Malawi wakitazama mchezo huo kati ya Nyasa Big Bullets na Yanga.

Mchezo huo uliohudhuriwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na mwenyeji wake Rais Dkt. Lazarus McCarthy Chakwera umepigwa kwenye uwanja wa taifa wa Bingu uliopo mji mkuu wa Malawi, Lilongwe.

Timu zote mbili zilishambuliana kwa zamu lakini hakuna iliyoibuka na ushindi hadi mwisho wa mchezo huku Yanga ikichezea sehemu kubwa ya wachezaji vijana na wengine wapya.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button