Nyumbani

Yanga sasa kuvuna milioni 20 kila bao

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametangaza dau la Sh milioni 20 kwa Yanga kama motisha kwa kila goli litakalofungwa katika mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Kiongozi huyo wa nchi ameongeza dau hilo kutoka Sh milioni tano katika michezo iliyopita hadi kiwango hicho.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa minara ya DTT iliyofanyika  ndani ya viwanja vya Azam Media, Tabata Dar es Salaam, Rais Samia amesema serikali itatoa ndege kwa ajili ya mashabiki watakaokwenda nchini Algeria kwa ajili ya mchezo huo.

Aidha ameipongeza Yanga kwa kutinga fainali ya shirikisho  ambapo atakutana na USM Alger ya Algeria.

Related Articles

Back to top button