Ligi Ya Wanawake

Yanga, JKT Quees kitawaka leo

LIGI Kuu ya Wanawake (WPL), inaendelea leo kwa michezo kadhaa kupigwa kwenye viwanja tofauti huku mtanange unaosubiriwa kwa hamu ukiwa kati ya Yanga Princess dhidi ya JKT Queens, utakaopigwa Uwanja wa Uhuru.

Mchezo mwingine utakuwa kati ya Mkwawa Queens dhidi ya Baobab Queens, Fountaine Gate Princess dhidi ya Ceasiaa.

Mpaka sasa JKT Queens inaongoza ligi ikiwa na pointi 37, ikifuatiwa na Simba Queens yenye pointi 36 na Fountain Gate Princess inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 35. Yanga Princess, inashika nafasi ya nne ikiwa na pointi 28.

Mpaka sasa kinara wa ufungaji mabao katika ligi hiyo ni Jentrix Shikangwa wa Simba Queens mwenye mabao 13, akifuatiwa na Donasia Minja wa JKT Queens mwenye mabao 12.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotlewa na Shirikisho la Soka TFF, kesho kutakuwa na mchezo mmoja kati ya Simba Queens dhidi ya Alliance Girls.

Related Articles

Back to top button