Mastaa

Wema Sepetu-Mimi si wa kwanza kukosa mtoto

DAR ES SALAAM:MSANII wa filamu nchini, Wema Sepetu, amewaomba mashabiki wake kuacha kumhurumia kuhusu suala la kukosa mtoto, akisema si yeye wa kwanza kupitia hali hiyo na anataka mjadala uelekezwe kwenye mambo mengine ya maisha.

Kupitia ukurasa wake wa Snapchat, Wema amechapisha ujumbe akieleza wazi msimamo wake na kusema tayari amekubali hali hiyo na kufanya amani na moyo wake.

“Ladies & Gentlemen, naomba nitoe tamko dogo… Msije mkadhani naumia, nooo! Matter of fact nimeaccept na nime-make peace na moyo wangu,” ameandika Wema.

Ameongeza kuwa hana sababu ya kuonewa huruma, kwani kukosa mtoto si jambo la kipekee kwake pekee.

“Msinionee huruma wapenzi… kwani mimi ni wa kwanza kukosa mtoto jamani? Aaah no bwana. Naomba mwaka huu tusemane kuhusu mambo mengine, sio mambo ya watoto,” amesema.

Msanii huyo pia amegusia maisha yake binafsi, akiwataka watu kuacha kuingilia masuala yanayomhusu ikiwemo kazi, nyumba na mali zake. Amesema urithi wa nyumba alioachiwa unatosha na hana presha ya kuthibitisha chochote kwa mtu yeyote.

“Maswali ya Wema hana kazi, hana nyumba sitaki. Urithi nilioachiwa wa nyumba unatosha. Nikijenga au nisipojenga, hiyo ni biashara yangu. Kwanza sina hata wa kumuachia urithi,” ameandika.

Amehitimisha ujumbe wake, Wema amesema anaelekea mwaka 2026 akiwa na mtazamo chanya wa maisha.
“Maisha ni mafupi, tuenjoy to the max. 2026 we living the good life, no questions asked,” amesisitiza.

Hii imejibu maswali yote ya mashabiki na uvumi waliokuwa wakisema Mitandaoni kuwa Wema ni mjamzito kitu ambacho sio kweli na picha za Mitandaoni ni za uongo.

Related Articles

Back to top button