Michezo Mingine

waendesha baiskeli kumuenzi Baba wa Taifa

kutoka Dar hadi Butiama kwa baiskeli

DAR ES SALAAM: Zaidi ya waendesha Baiskeli 200 kutoka nchini na nchi mbalimbali kushiriki msafara wa Twende Butiama kumuenzi Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Lengo la ushiriki ni kuendeleza falsafa ya  Mwalimu Nyerere juu ya Elimu,Afya na utunzaji wa mazingira

Mkuu wa Msafara wa Twende Butiama Gabriel Landa amesema msafara huo utamuenzi Baba wa Taifa kwa vItendo kwa kupambana na maadui wa maendeleo  ambao ni Ujinga, umaskini na maradhi.

Amesema Msafara huo unatarajia kupita zaidi ya Mikoa 12 ambapo watashiriki na watanzania wengine katika kumbukizi ya kifo cha miaka 25 cha Baba wa Taifa tangu alipofariki.

Pia, Gabriel amesema msafara huo ni kilomita 1,846 kutoka Dar es salaam mpaka Butiama huku  wakitegemea kupata washiriki kutoka maeneo mbalimbali ya Tanzania na washiriki kutoka nchi za jirani  kama Zimbabwe, Afrika Kusini, pamoja na Namibia, lengo likiwa kuwaleta pamoja watanzania na Waafrika ili kuishi na kumuenzi Baba wa Taifa.

Sambamba na hayo amesema kuwa kwenye msafara huo watapeleka ujumbe wa kuchangia madawati ikiwa ni kampeni waliyoanza kuitekeleza tangu mwaka 2021 na mwaka huu wanategemea kuwa na madawati zaidi ya 500  ambayo watayagawa katika shule mbalimbali.

 

Related Articles

Back to top button