Africa

“Viongozi tumeumizwa na matokeo”

MWANASHERIA wa klabu ya Yanga Simon Patrick amesema matokeo ya mchezo wa michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kufuzu hatua ya makundi dhidi ya Club Africain yamewaumiza viongozi wa timu hiyo ya Jangwani.

Timu hizo zilitoka suluhu katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram Patrick ameandika kwamba wanachokifanya mashabiki wa Yanga kutoa ya moyoni ni sahihi kabisa kwani ndiyo haki kubwa waliyonayo.

“Kama Viongozi tumeumizwa sana na matokeo ya jana ukizingatia tumefanya kila kitu kiutendaji kwa ajili ya kuwafurahisha mashabiki wetu lakini mambo hayakwenda kama tulivyotarajia,” amesema Patrick.

Amesema uongozi wa Yanga ni sikivu sana, umepokea na unaendelea kupokea maoni na ushauri wa mashabiki, watayachakata na kuyafanyia kazi.

Kiongozi huyo amesema Rais wa klabu hiyo na Kamati ya Utendaji wamejitahidi kuhakikisha Yanga ina kila kitu kinachohitajika kwa ajili ya timu, lakini matokeo yamekua kinyume na matarajio.

Amewaomba mashabiki kuendelea kuisapoti timu hiyo kwenye mchezo wa marudiano utakaofanyika Novemba 9, Tunisia.

Related Articles

Back to top button