Featured

Vialli afariki dunia

MSHAMBULIAJI wa zamani wa timu ya taifa ya Italia ‘Azzurri’, klabu za Chelsea na Juventus, Gianluca Vialli amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 58.

Vialli amefariki dunia kufuatia miaka mitano ya mapambano dhidi ya saratani ya kongosho.

Amefariki dunia hospitali mjini Londonki wiki chache tu baada ya vifo vya wachezaji wa zamani Sinisa Mihajlovic wa Serbia na Edson Arantes do Nascimento ‘Pele’ wa Brazil mwezi uliopita.

“Tunawashukuru wengi waliomsaidia kwa miaka mingi kwa upendo wao. Kumbukumbu na mfano wake vitaishi milele katika mioyo yetu,” imesema taarifa ya familia ya Mihajlovic.

Vialli aliiwakilisha Azzurri michuano ya Kombe la Dunia mwaka 1986 na 1990, alishinda Ligi ya Mabingwa akiwa Juventus mwaka 1996 na alipata umaarufu England alipocheza Chelsea kwa kipindi kifupi.

Aliitumikia Chelsea akiwa Kocha mchezaji na kisha kocha kamili akiiongoza timu hiyo kutwaa Kombe la Washindi Ulaya na Kombe la Ligi mwaka 1998 pamoja na kombe la FA mwaka 2000.

Related Articles

Back to top button