EPL

Usajili mpya Man City kuionja Chelsea leo

MANCHESTER: Kocha mkuu wa Manchester City Pep Guardiola amesema wachezaji wake wapya waliosajiliwa dirisha hili la Januari Vitor Reis, Abdukodir Khusanov na Omar Marmoush wako tayari kukitumikia kikosi hicho kwenye mchezo wa baadaye dhidi ya Chelsea.

Alipoulizwa na mwandishi wa habari iwapo angewatumia wachezaji hao katika mchezo wa leo dhidi ya Chelsea Guardiola alijibu wako tayari na anaweza kuwatumia wote

“Ndio, wanaweza kucheza na wako tayari. Tuna upungufu wa wachezaji, tuna Omar ambaye ana sifa za kipekee ubora wake eneo la mwisho ni hazina ya kipekee kwa kikosi chetu kwa miaka mingi ijayo. Amesema Pep

Manchester City wanaialika Chelsea dimbani Etihad leo kuanzia saa 2:30 usiku huku wakiwakosa winga wao wa kushoto Jeremy Doku na beki wa kati Ruben Diaz kutokana na majeruhi.

Related Articles

Back to top button