Michezo MingineSoka La Ufukweni
Usafiri pasua kichwa, safari ya timu ya taifa soka la ufukweni

KIKOSI cha timu ya Taifa ya Soka la Ufukweni kinaendelea na maandalizi katika fukwe za Coco Dar es Salaam kuelekea msimu wa pili wa mashindano ya Afrika (Africa Beach Games)yatakayofanyika nchini Tunisia kuanzia Juni 24- 30.
Wakati timu hiyo ikiendelea kujifua bado kumekuwa na changamoto ya kupata usafiri utakaowapeleka Tunisia kutokana na ndege kujaa.
Katibu mkuu wa kamati ya Olimpiki Tanzania Filbert Bayi amesema kwasasa wanapambana kupata usafiri ambapo Tanzania inatarajiwa kupeleka timu ya riadha pamoja na timu ya soka la Ufukweni.
Endapo taratibu za usafiri zitakaa sawa timu hiyo inatarajiwa kuondoka nchini Juni 24 kwa ajili ya michuano hiyo.