Umri ni namba tuu unabisha? Waulize Milan

WAHENGA waliwahi kusema kijiji hakikosi wazee, lakini wahenga hao hao walisema wazee ni hazina, hivi ndivo ilivyo kwasasa kwa kikosi cha Inter Milan ambacho kimebakiza hatua chache kutinga fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya ushindi wa bao 2-0 dhidi ya pacha wao AC Milan.
Mkongwe Edin Dzeko mwenye miaka 37 alikuwa wa kwanza kuziona nyavu za AC Milan kwenye dakika ya 8 ya mchezo, kisha mkongwe mwingine Henrikh Mkhitaryan (34) akapigilia msumari wa pili na wa mwisho kwenye dakika ya 11 ya mchezo huo.
Inter Milan wanasaka kucheza fainali yao ya kwanza ya ligi ya mabingwa barani Ulaya kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2010 walipotwaa ubingwa wakiwa na kocha mtukutu Jose Mourinho aliyekuwa na moja ya kikosi bora kuwahi kutokea kwenye timu hiyo.