Ligi Kuu

‘Uliyemgoja kaja’

DAR ES SALAAM: PAZIA la Ligi Kuu Bara msimu wa 2024/25 linakwenda kufunguliwa kesho Agosti 16, mwaka, kwa mchezo mmoja, Pamba Jiji FC dhidi ya Tanzania Prison, mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

Mechi zingine Agosti 17, Mashujaa FC watawakaribisha Dodoma jiji uwanja wa Lake Tanganyika na Namungo watawakaribisha Fountain Gate katika dimba la Majaliwa, Ruagwa, Lindi.

Simba itakuwa nyumbani na kutumia uwanja wa KMC uliopo Mwenge, jijini Dar es Salaam dhidi ya Tabora United, mchezo utachezwa Jumapili ya Agosti 18 na Singida Black Stars watatupa karata yake ya kwanza ugenini dhidi ya Ken Gold, dimba wa Sokoine Mbeya.

Mabingwa watetezi wa Ligi, Yanga wakitwaa taji hilo mara 30, watakuwa kibarua cha mchezo wa awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Agosti 17, mwaka huu, wakicheza ugenini kusaka ushindi dhidi ya Vital’O ya Burundi.

Mchezo huo utachezwa uwanja wa Azam Complex, jijini Dar es Salaam baada ya Vital’O kuchangua dimba hilo kama uwanja wa nyumbani baada ya nchini kwao kutokidhi vigezo vya CAF.

Katika michezo ya Ligi Kuu, Yanga watakuwa na kibarua Agosti 29, 2024, watakuwa ugenini dhidi ya Kagera Sugar, kwenye dimba la Kaitaba, Kagera.

Related Articles

Back to top button