Habari Mpya

Tuzo za TFF 2024/25: Mashabiki, Klabu kukumbukwa

DAR ES SALAAM: RAIS wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema wanafanya maboresho ya tuzo kwa msimu wa 2024/25 wataweka zawadi ya mashabiki bora na klabu inayoingiza mapato mengi kwenye mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara

Karia amezungumza hayo muda mchache kabla ya kuanza ugawaji wa tuzo kwa wanamichezo na timu bora waliofanya msimu uliopita wa 2024/25 hafla iliyofanyika katika ukumbi wa The Super Dome Masaki jijini Dar es Salaam.

Karia amesema baada ya kufanikiwa kutoa tuzo katika nafasi mbalimbali msimu ujao wataboresha na kuweka vipengele vya klabu inaoingiza mashabiki wengi na mapato makubwa.

“Tutashundanisha mashabiki bora walioingia uwanjani kwa wingi na kuingiza mapato makubwa, licha ya fedha hizo kwenda katika klabu yenyeji,” amesema Karia.

Ameongeza kuwa maboresho hayo ni kuwapa nguvu zaidi mashabiki ambao hujitokeza uwanjani kwa wingi kusapoti timu zao zinapokuwa uwanjani.

Ikumbukwe Novemba12,2023, Simba iliwahi kutwaa tuzo ya mashabiki bora katika michuano ya AFL, ambayo rasmi yalizinduliwa nchini Tanzania katika dimba la uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam.

Related Articles

Back to top button