Kwingineko

Trump kuhudhuria fainali CWC

WASHINGTON: Rais wa Marekani Donald Trump, amesema atahudhuria katika mchezo wa fainali ya Kombe la Dunia la Klabu utakaopigwa katika dimba la MetLife Stadium liliopo jijini New Jersey Jumapili baada ya shirikisho la soka duniani FIFA kutangaza kufungua ofisi katika jengo lake la Trump Tower jijini New York

Trump ametangaza uamuzi huo katika kikao cha baraza la mawaziri jana Jumanne jioni Katika hatua inayotafsiriwa na wengi kama hatua ya Rais huyo mfanyabiashara kulipa fadhila kutokana na kitendo cha FIFA kufungua ofisi katika jengo lake.

Michuano hiyo iliyopanuliwa inayoshirikisha klabu bora zaidi duniani imeonekana kutabiri mabaya kwa Kombe la Dunia la 2026, ambalo litaandaliwa kwa pamoja na Marekani, Canada na Mexico kutokana na mwamko mdogo wa mashabiki na hali ya hewa ambayo mara nyingi imekuwa ikitatiza michezo mbalimbali.

Katika tangazo la kufungua ofisi kwenye jengo la Trump Tower, Rais wa FIFA Gianni Infantino alitangaza pia uwepo wa taji la ubingwa la kombe la Dunia la Klabu litakalokuwepo hapo hadi siku ya fainali jumapili wiki hii ambapo watu mbalimbali watapata fursa ya kuliona na kupiga picha.

Trump hajakwepa jukwaa la michezo wakati huu wa muhula wake wa pili kwani amekuwa Rais wa kwanza aliye madarakani kuhudhuria mchezo wa Super Bowl mwezi Februari.

Ukandamizaji wake wa uhamiaji na kupiga marufuku kusafiri kwa nchi 12 kumezua wasiwasi kuelekea Kombe la Dunia la mwaka ujao hata hivyo Infantino ametoa hakikisho kwamba ulimwengu utakaribishwa nchini Marekani wakati utakapofika.

Related Articles

Back to top button