Ligi KuuNyumbani

TFF yazifungia Singida, Prisons kusajili

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF) limezifungia kusajili klabu za Ligi Kuu Tanzania Bara za Tanzania Prisons na Singida Big Stars kwa kosa la kusajili wachezaji wenye mikataba na klabu nyingine.

Taarifa ya TFF imesema uamuzi huo umefanywa wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya shirikisho hilo kwa kuzingatia kanuni ya 47(210 ya Ligi Kuu baada ya kuzikuta na kosa hilo.

Adhabu hiyo ni kwa dirisha moja la usajili.

Kipa wa Coastal Union, Musa Mbise.

Tanzania Prisons ilimsajili kipa Musa Mbise wa Coastal Union wakati ikifahamu kuwa bado ana mkataba na klabu hiyo.

Nayo Singida Big Stars ilimsainisha mkataba kipa Metacha Mnata huku akiwa bado ana mkataba na klabu ya Polisi Tanzania.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button