Tetesi za usajili Ulaya

KLABU ya Arsenal inapanga kufanya jaribio la kumsajili nyota wa Brentford ‘The Bees’ Ivan Toney Januari, 2024. The Bees inaaminika kuthamini mshambuliaji huyo kwa pauni milioni 60 sawa na shilingi bilioni 180.7. (Mirror)
Luka Modric ameibuka kuwa mlengwa wa usajili wa timu ya Inter Miami ya Marekani ya David Beckham ambako Lionel Messi, Jordi Alba na Sergio Busquets wote wamejiunga nayo majira ya kiangazi.(The Dubrovnik Times)
Pia Marc Cucurella anataka kuondoka Chelsea muda mfupi ujao kutokana na kushindwa kupata nafasi ya kucheza msimu huu. Real Madrid imekuwa ikifuatia hali yake Stamford Bridge.(The Sun)
Xabi Alonso anatarajiwa kuwa kocha wa Real Madrid msimu ujao licha ya kuiongoza Bayer Leverkusen chini ya mwaka mmoja. (Radio Marca)
Manchester United na Newcastle United zinagombea saini ya kiungo wa Juventus, Adrien Rabiot.(Sky Sports)