Tetesi

Tetesi za usajili

TIMU ya Chelsea imemweka mshambuliaji wa Napoli, Victor Osimhen kuwa kipaumbele chake wakati wa dirisha la usajili la majira ya kiangazi 2024 na huenda tayari imefikia makubaliano ya kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa Nigeria.(Football Transfers)

Mshambuliaji mwingine aliyeko katika rada za Chelsea ni Ivan Toney wa Brentford, huku mazungumzo yanaendelea kuhusu uwezekano wa uhamisho Januari 2024.(football.london)

Lakini Liverpool ina nia kushindana na Chelsea kupata saini ya Toney na pia Arsenal imeonesha nia kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27.(Fichajes)

Klabu ya Trabzonspor ya Uturuki ipo katika harakati za kumsajili kiungo wa Liverpool, Thiago Alcantara kabla ya dirisha la usajili la nchi hiyo kufungwa Septemba 15.(Aksam)

Tottenham Hotspur inamfuatilia fowadi wa Sporting CP, Pedro Goncalves kabla ya uwezekano wa kutuma ofa Januari 2024, lakini italazimika kukabiliana na upinzani kutoka kwa Aston Villa, Newcastle United na Liverpool.(O Jogo)

Liverpool na Manchester United zote zimetumia kipindi cha michezo ya kimataifa kuwafuatalia mabeki nyota mreno Antonio Silva wa Benfica na mtaliano Giorgio Scalvini wa Atalanta.(90min)

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button