Kwingineko

Ter Stegen ajipa miezi mitatu Barca

BARCELONA: Nahodha wa mabingwa wa Laliga FC Barcelona na kipa wa timu ya taifa ya Ujerumani Marc-Andre ter Stegen kupitia ukurasa wake wa Instagram ametangaza kuwa atakuwa nje ya uwanja kwa muda wa miezi mitatu akijipa muda kupata nafuu wa kupata nafuu kutokana na upasuaji wa mgongo.

Ter Stegen mwenye miaka 33 hakuwa uwanjani kwa miezi saba baada ya kupata jeraha la goti mwaka jana ambalo lilimlazimu kufanyiwa upasuaji kabla ya kurejea mwezi Mei. Kabla ya hapo alifanyiwa upasuaji wa mgongo mwaka 2023 ambao ulimuweka nje kwa zaidi ya miezi miwili.

Ter Stegen ambaye amekuwa Barcelona tangu 2014 amesema katika chapisho hilo kuwa wakati huu madaktari wake wanaamini kuwa takriban miezi mitatu itahitajika kama tahadhari ili kukwepa hatari yoyote.

“Kihisia inaniuma sana kutoweza kusaidia timu wakati huu. Kwa bahati nzuri naweza kumudu kukaa sawa kwa muda mfupi na naona njia ya kurudi uwanjani iko wazi.” – alisema kipa huyo aliyeshinda mataji sita ya LaLiga na Ligi ya Mabingwa akiwa na klabu hiyo.

Related Articles

Back to top button