Taylor Swift, Travis Kelce wazua gumzo harusini

NEW YORK: MWANAMUZIKI Taylor Swift na Travis Kelce wamezua gumzo kwenye mitandao ya kijamii wakati wakiwa katika harusi huku Taylor akiwa amemlalia Travis begani huku akionyesha mahaba.
Wawili hao ni wanandoa waliohudhuria harusi ya binamu wa Travis, Tanner Corum, ambaye alifunga pingu za maisha na Samantha Peck. Picha hizo zinaonesha Taylor akiwa amevalia vazi lenye maua ya samawati huku Travis akivalia shati na suruali ya mikono mirefu.
Katika moja ya picha hizo, Taylor anaonekana akiegemeza kichwa chake kwenye bega la Travis huku wakiitazama kamera iliyoashiria kwamba walipiga picha hiyo kwa kupenda na hakuna kificho chochote kuonyesha mapenzi yao kwa jamii.
Video nyingine iliyosambaa mitandaoni inamuonesha bibi na bwana harusi wakicheza muziki wa kimahaba huku Taylor na Travis wakiwawasindikiza kwa macho na tabasamu wakiwa wameketi pamoja kwenye viti vyao.
Baadhi ya mashabiki waliofurahishwa na picha na video zao wamewasifia wanandoa hao wakiwatakia maisha memba yenye furaha katika mapenzi yao: “Nzuri sana kuwaona wote wawili, ninapenda mitindo yao ya nywele.” Mwingine aliandika, “Wanaonekana wazuri sana pamoja na Taylor anaonekana mrembo hasa.
Shabiki mwingine aliandika; “Ninapenda jinsi wanavyoonekana kawaida! Natumai wamekuwa wakifurahia wakati wao pamoja.”
Taylor na Travis walithibitisha mapenzi yao kwa mara ya kwanza Septemba 2023, mwimbaji huyo alipohudhuria mchezo wake wa kwanza wa Kansas City Chiefs katika Uwanja wa Arrowhead.
Swift amehudhuria michezo kadhaa ikiwemo kandanda na Super Bowls kwa mwaka 2024 na 2025, huku Travis akizunguka duniani kote kumuunga mkono mwimbaji huyo wakati wa Ziara yake ya Eras, iliyohitimishwa Desemba 2024.