Tanzania yaichapa Rwanda michuano ya Kwibuka

KIGALI:TIMU ya wanawake ya Kriketi ya Tanzania imeichapa Rwanda kwa mikimbio 78/3 dhidi ya 74/10, michuano ya Kwibuka katika mchezo uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Gahanga, Kigali.
Kwa matokeo hayo, Tanzania imeshinda kwa wikets 7.
Katika mchezo huo, Merveille Uwase wa Rwanda alijitahidi kwa kuweka alama 22 akicheza kwa overs 33, lakini alishindwa kuongoza timu yake kwa ushindi.
Agnes Qwele alipata alama 4/7 akiwa na overs 4 na kuibuka mchezaji bora kwa kufanya vizuri katika mchezo huo.
Kwa upande wa Tanzania, Fatuma Kibasu aliongoza kwa kiwango cha juu, akiendelea kuwa imara kwenye lango, akibaki bila kupoteza akipata overs 37. Kibasu alionesha ufanisi wa kipekee, akiwa na mchango mkubwa kwenye ushindi wa timu yake.
Henriette Ishimwe, mchezaji wa Rwanda, alijitahidi kuweka alama ya 2/15 kwa overs 2.2, lakini alikosa msaada kutoka kwa wachezaji wenzake ili kuzuia ushindi wa Tanzania.
Tanzania inayoshika nafasi ya nne imebakiza mchezo mmoja dhidi ya Cameroon utakaochezwa kesho ambao utaamua kama atatinga hatua ya nusu fainali.