Afrika Mashariki
Tanzania U18 yapoteza

TIMU ya Taifa ya mpira wa Miguu kwa vijana chini ya miaka 18 imeonja joto ya jiwe baada ya kupoteza mechi dhidi ya Sudan Kusini kwa mabao 2-1 katika michuano ya Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati(CECAFA) inayoendelea Kenya.
Tanzania itacheza mchezo wa mwisho wa kundi B dhidi ya Zanzibar Desemba 2, 2023.
Katika mchezo wa kwanza Novemba 26, Tanzania iliifunga Uganda bao 1-0.