Tanzania Comedy Awards Kufanyika Kesho Februari 22, 2025

DAR ES SALAAM:KAMATI ya Maandalizi ya Tanzania Comedy Awards (TCA) kwa kushirikiana na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) na Bodi ya Filamu, chini ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, wametangaza utaratibu rasmi wa usiku wa ugawaji wa tuzo hizo.
Tukio hilo litafanyika kesho, Jumamosi, Februari 22, 2025, na litakuwa na utaratibu ufuatao:
Muda wa Kuingia: 10:00 – 11:30 jioni (Baada ya muda huo, hakuna atakayeruhusiwa kuingia)Muda wa tuzo Kuanza: Sherehe itaanza rasmi saa 12:00 jioni
Wageni Maarufu: Wanaombwa kuzingatia usalama, hawataruhusiwa kuingia na walinzi wao.
Mavazi ya heshima na Inashauriwa kuvaa mavazi ya heshima yanayoendana na tukio hili kubwa litakalohudhuliwa na viongozi mbalimbali na watu maarufu.
Mgeni rasmi wa hafla hiyo atakuwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye atahudhuria kwa heshima ya tasnia ya uchekeshaji nchini.
Tanzania Comedy Awards ni jukwaa la kutambua na kuthamini mchango wa wachekeshaji wa Tanzania katika burudani na sanaa. Usiku huu unatarajiwa kuwa wa kipekee kwa wadau wa tasnia hiyo.




