
WATAALAMU na wadau wa muziki Barani Afrika watakutana Tanzania kubadilishana mawazo ambapo pia maonesho ya muziki wa Afrika yatafanyika Novemba 24-26, 2022.
Matukio hayo yatafanyika Dar es Salaam.
Mkutano wa wataalamu na wadau hao yatafanyika katika ukumbi wa Julius Nyerere wakati maonesho ya muziki yatafanyika eneo la Makumbusho.